Miradi mikubwa ya mafuta ya visukuku kama hii haiwezi kuendelea bila fedha za benki, watoaji bima na wawekezaji matajiri - wengi wao wakiwa Ulaya, Marekani Kaskazini na Asia Mashariki. Benki ya Deutsche ni mfadhili wa tano kwa ukubwa barani Ulaya wa mafuta ya visukuku na ni mojawapo ya benki pekee za Ulaya ambazo bado zimejiandaa kufadhili bomba la EACOP. Hii inabidi ibadilike.
Wasimamizi nchini Uganda na Tanzania wamekuwa wakipigana kusitisha Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki na wanaungwa mkono na watu duniani kote. Wanaharakati wa Uganda hivi karibuni walizuru Ulaya na kukutana na maelfu ya wanakampeni wenzao huko Berlin na Paris, wanasiasa, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, na hata Papa Mtakatifu - ambao wote wanaunga mkono kampeni hii. Sisi pia tunaweza kushikamana na kuwaunga mkono katika mapambano yao kwa kuhakikisha kuwa Total haipati fedha na kulazimishwa kusimamisha upanuzi wa mafuta ya visukuku.
Kadiri athari za mzozo wa hali ya tabianchi, janga (la Corona), kupanda kwa bei ya maisha na nishati, na mizozo mengine kama vita vya Ukraine kuanza kugonga sana, ni wazi kwamba sasa zaidi ya hapo awali, tunahitaji kuhama haraka kutoka kwa uchumi unaotegemea mafuta ya visukuku. Benki ya Deutsche inahitaji kuamua kama wanataki kubaki kuwa tatizo, au kama wanataka kuwa suluhisho kwa kuwekeza katika mpito wa nishati salama, safi na nafuu zaidi kwa wote. Wana fursa ya kufanya hivyo kwa kutangaza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) yao ijayo Mei 19 kwamba hawatatoa fedha kwa ajili ya bomba la EACOP na upanuzi wa mafuta ya visukuku. Hadi wakati huo, tuhakikishe kwamba wanasikia ujumbe wetu.