Tuna ahidi kuunda kwa haraka dunia isiyokuwa na visukuku.
Kwa kutenda kazi pamoja,tutakomesha matumizi ya visukuku na kuhamisha dunia yetu kwa asilimia mia moja ya nishati safi, kwa wote. Na tunatoa wito kwa wanasiasa kufuata uongozi wetu.
Tunaishi katika miaka ya joto kabisa ya historia ya binadamu. Vimbunga,mafuriko na ukame zilizozidi zinazoharibu makao na mataifa. Janga la tabia nchi sio tishio la baadaye tena: ni hatari iliyo wazi na ya sasa.
Bado tunaona matumaini mapya kila mahali. Katika kila nchi, watu wa kawaida wanaonyesha uongozi barabara wa tabia nchi kwa kuongea kinyume na miradi ya makaa mawe, mafuta na gesi, kutoa pesa zao kutoka kwa visikuku na kujenga nishati safi kwa wote.
Miaka miwili iliyopita mjini Paris, Ufaransa, serikali za dunia waliweka ahadi ya kihistoria, kulinda makao yetu sote na kuyaweka kwa joto linaloishika. Lakini matendo yao hayakufanana na maneno hayo. Nchi zinaendelea kupitisha miradi mapya ya makaa mawe, mafuta na gesi, na kudhamini mabilioni katika visukuku.
Hivyo ni juu yetu kupinga viwanda fisadi vya visukuku, wanasiasa na washirika wao wa kifedha na kutengeneza mabadiliko ya ukweli tunayotafuta. Matarajio yetu ni ya kimataifa na itachukua sisi sote kutenda kwa pamoja nchini, ili kuunda baadaye ya Fossil Free tunayohitaji.